Pata taarifa kuu
EBOLA-SIERRA LEONE-SHERIA

Ebola : hatua kali zachukuliwa Sierra Leone

Jumatano, Sierra Leone imeamuru kufungwa kwa muda wa siku tano sehemu zote kunakokusanyika watu kaskazini mwa nchi hiyo.

Kituo cha matibabu dhidi ya virusi vya Ebola katika mji wa Freetown, Sierra Leone.
Kituo cha matibabu dhidi ya virusi vya Ebola katika mji wa Freetown, Sierra Leone. Reuters/Umaru Fofana
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imechukulia ili kuzuia kuenea kwa virusi vya Ebola katika eneo hilo la kaskazini hususan kwa watu wanaotafutwa na vyombo vya sheria.

Jumanne Desemba 23, kwa mara ya kwanza, mkuu wa kimila alihukumiwa kifungo cha miezi sita jela kwa kuificha serikali kuwa jamaa zake waliambukizwa virusi vya Ebola.

Hukumu hii inaonekana kuwa kali kwa mtu ambaye alipoteza mke wake na binti yake kutokana na virusi vya Ebola. Lakini, kwa mujibu wa viongozi, ilikuwa vizuri kutoa ujumbe wa wazi kwa raia.

Mkuu wa kimila, Amadu Kargbo, alipoteza mke wake na binti yake kutokana na virusi vya Ebola. Vyombo vya sheria vinamtuhumu kuwa alificha ugonjwa uliyokua ukiiathiri familia yake na kupelekea viongozi wa serikali za mitaa na viongozi wa Idara ya afya kuwa na mashaka kufuatia vifo hivyo. Mkuu huyo wa kimila anatuhumiwa pia kuwazika jamaa zake kwa siri, na kufanya mazishi yasiyo salama katika eneo analoongoza la Bumpeh, kilomita 120 kutoka Freetown.

Kwa mujibu wa viongozi, hukumu yake ambayo inaweza kuonekana kali, itapelekea ujumbe fulani kwa raia ili waweze kuwa makini kama alivyothibitisha Sidi Yayhya Tunis msemaji wa Idara ya kupambana dhidi ya Ebola.

" Visa vya wagonjwa wa Ebola vinaendelea kuenea, hasa kwa sababu watu wamekua wakiwazika siri ndugu zao kwa siri au kuwaficha makwao ndugu zao wanaoathirika na Ebola.Tumehamasisha raia. Lakini unajua, wakati mwingine hatua kali zinahitajika ili kukomesha ukiukwaji wa sheria, ukiukwaji ambao umekua ukiongezeka kutokana na hali ya kutoadhibu ambayo imekithiri Sierra Leone", amesema Sidi Yayhaya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.