Pata taarifa kuu
DRC-M23-KENYA-RWANDA-UGANDA-WAKIMBIZI-MAKUBALIANO

Serikali ya DRC yaendelea kulaumiwa

Ni mwaka mmoja sasa tangu serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo itie saini kwenye Azimio la Nairobi ambalo limeahidi kukomesha mapigano kati yake na waasi wa zamani wa M23 na kuwataka waasi hao kurudi nchini DRC baada ya kupewa msamaha.

Joseph Kabila, rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambaye serikali yake inalaumiwa kutotekeleza makubaliano kati yake na waasi wa zamani wa M23 yaliyoafikiwa mjini Nairobi, Kenya.
Joseph Kabila, rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambaye serikali yake inalaumiwa kutotekeleza makubaliano kati yake na waasi wa zamani wa M23 yaliyoafikiwa mjini Nairobi, Kenya. REUTERS/James Akena
Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa hatua nyingine zilizochukuliwa ni pamoja na baadhi ya wapiganaji hao wa zamani kufunguliwa mashtaka kwa uhalifu wa kivita na ukiukwaji wa haki za kibinadamu.

Mwaka mmoja baada ya Azimio hilo, ufinyu wa utekelezwaji wa makubaliano hayo unawafanya wachambuzi wa masuala ya siasa za kiukanda kuhoji ikiwa serikali ya Joseph Kabila ina dhamira ya dhati kuhakikisha makubaliano hayo yanatekelezwa.

Hata hivyo, Ujumbe maalum wa serikali ya Congo unatarajiwa kuwasili Ijumaa wiki hii mjini Kigali kuanzisha ratiba ya kuwarudisha waasi waliokimbilia nchini Rwanda baada ya ziara kama hiyo kuahirishwa mara mbili.

Kwa upande wa Uganda, licha ya serikali nchini humo kutishia hapo awali kutoa hadhi ya ukimbizi wa kisiasa kwa waasi hao ifikapo Desemba 12 mwaka huu ikiwa serikali ya Kinshasa itashindwa kuwarejesha nchini DRC, hataimaye Alhamisi wiki hii msemaji wa serikali ya Uganda alisema serikali yake itasubiri kutoa hadhi hiyo ya ukimbizi kwa kuhofia kuhatarisha mchakato wa amani.

wapiganaji wa kundi la waasi wa zamani la M23, Februari mwaka 2014.
wapiganaji wa kundi la waasi wa zamani la M23, Februari mwaka 2014. AFP PHOTO/ ISAAC KASAMANI

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.