Pata taarifa kuu
UN-WAKIMBIZI-MSAADA

UN yatiwa hofu na hali inayowakabili wakimbizi

Mkuu wa tume ya Umoja wa Mataifa inayoratibu misaada, Valerie Amos , amesema zaidi ya dola milioni 16 zinahitajika kusaidia harakati za Umoja wa Mataifa duniani kwa mwaka ujao, kufadhili shughuli za kimisaada kwa mamilioni ya watu wanaokimbia mapigano duniani.

Mkuu wa tume ya Umoja wa Mataifa inayoratibu misaada, Valerie Amos , amesema zaidi ya dola milioni 16 zinahitajika kusaidia harakati za Umoja wa Mataifa duniani
Mkuu wa tume ya Umoja wa Mataifa inayoratibu misaada, Valerie Amos , amesema zaidi ya dola milioni 16 zinahitajika kusaidia harakati za Umoja wa Mataifa duniani REUTERS/Swoan Parker
Matangazo ya kibiashara

Amos amefahamisha kuwa nusu ya fedha hiyo inahitajika nchini Syria pekee.

Ripoti ya Umoja wa Mataifa imesema raia wa Syria wapatao milioni tatu wamelazimika kuyahama makazi yao kukimbia mapigano yanayoendelea na kukimbilia nchi jirani, na wengine milioni kumi na mbili wakiwa wametawanyika nchini humo.

Wakati hayo yakijiri Shirika la Umoja wa Mataifa linalowahudumia watoto duniani, UNICEF limesema mwaka 2014 ulijaa vitisho, majanga na kukatishwa tamaa kwa mamilioni ya watoto duniani.

Katibu mtendaji wa shirika hilo, Anthony Lake amesema mwaka 2014 ulishuhudia mizozo ikizidi kushika kasi maeneo mbali mbali duniani, watoto wakilengwa kutumikishwa na vikundi vilivyojihami huku dunia nayo ikisahau majanga mengine.

Lake amesema takribani watoto milioni 230 duniani kote wameathirika na majanga yanayoendelea duniani bila kusahau mlipuko wa Ebola unaoendelea kushuhudiwa Afrika Magharibi. Wengine wameuawa wakiwa madarasani au wamelala, na wengine wakishuhudia wazazi wao wakiuawa.

Watoto wakisoma magazeti yanayozungumzia Ebola, magazeti ambayo yalizambazwa UNICEF nchini Liberia.
Watoto wakisoma magazeti yanayozungumzia Ebola, magazeti ambayo yalizambazwa UNICEF nchini Liberia. Unicef

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.