Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-Katiba-Siasa

Burkina Faso: rasimu ya mkataba "msingi" wa ufumbuzi wa mgogoro

Rais wa Umoja wa Afrika, msuluhishi akiwa pia rais wa Mauritania, Mohamed Ould Abdel Aziz, alikutana Jumatatu Novemba 10, mjini Ouagadougou na wadau wote katika mgogoro wa Burkina Faso. Kwa upande wake upinzani umewasilisha mkataba wao kwa jeshi katika hali ya kuundwa kwa taasisi za mpito.

rais wa Mauritania, akiwa pia rais wa Umoja wa Afrika, Mohamed Ould aAbdela Aziz, wakati wa mkutano na luteni kanali Zida pamoja na viongozi wa upinzani, viongozi wa kidini na kimila, mjini Ouagadougou, Novemba 10 mwaka 2014.
rais wa Mauritania, akiwa pia rais wa Umoja wa Afrika, Mohamed Ould aAbdela Aziz, wakati wa mkutano na luteni kanali Zida pamoja na viongozi wa upinzani, viongozi wa kidini na kimila, mjini Ouagadougou, Novemba 10 mwaka 2014. AFP PHOTO / ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Mohamed Ould Abdel Aziz, ambae hawakuwa na ushirikano mzuri na aliye kuwa rais Burkina Faso, Blaise Compaoré, amesema mwanzoni kwamba Umoja wa Afrika haukuja "kuifanyia vitisho " Burkina Faso au "kuilazimisha" kitu chochote.

“ Tuko hapa ili kusaidia ndugu zetu wa Burkina Faso ili kupitia mchango wa kila mmoja waweze kupatia ufumbuzi matatizo yanayoikabli nchi yao”, amesema rais wa Umoja wa Afrika.

Hata hivo Jumatatu Novemba 3, Umoja wa Afrika ulibaini kwamba utalichukulia vikwazo jeshi, iwapo halitokabidhi madaraka kwa raia mnamo siku 15.

Vitisho hivyo vilipokelea vibaya mjini Ouagadougou. Luteni kanali Yacouba Isaac Zida, wajumbe wa vyama vya kiraia na upinzani walisema juma liliyopita kwamba Umoja wa Afrika uliharakia kutoa vito vitisho hivyo. Lakini Jumatau Novemba 10, upinzani ulielezea furaha yake kuona Umoja wa Afrika unaendelea na jitihada za kutafutia suluhu mgogoro nchini Burkina Faso.

Upinzani na vyama vya kiraia viliwasilisha rasimu ya mkataba wao kwa jeshi katika hali ya kuundwa kwa taasisi za mpito. Wakati huohuo Luteni kanali Yacouba Isaac Zida anaye shikilia wakati huu madaraka ya uongozi wa nchi, amesema rasimu hiyo ya mkataba ni “msingi” wa ufumbuzi wa mgogoro.

Rasimu ya mkataba huo iliyopitishwa bila kupingwa imependekeza kuundwa kwa serikali mpya itakayo kuwa na wajumbe 25 kufuatia hali inayojiri wakati huu nchini Burkina Faso.

Wajumbe kutoka vyama vya siasa, vyama vya kiraia, viongozi mbalimbali wa kidini na viongozi wa kimila waliafikiana kuundwa kwa serikali hiyo mpya itakayojumuisha pande zote husika katika mgogoro unaoendelea nchini humo.

Bunge litaundwa na Wabunge 90. Bunge hilo litaundwa kwa kuzingatia vyama viliyokua karibu na utawala wa zamani wa Blaise Compaoré. Upinzani utapata viti 40, vyama vya kiraia vitakua na viti 30, jeshi litakua na viti 10 pamoja vyama vingine vya saiasa visiyoegemea upande wowote vitapata viti 10.

Wajumbe wote wa Bunge la mpito wanaweza kugombea katika chaguzi zijazo. Hata hivyo rais , Waziri mkuu na wajumbe wa serikali ya mpito hawataweza kugombea katika chaguzi zijazo, ambazo zitafanyika baada ya serikali ya mpito.

Ili kuepuka mgogoro mwingine kama ule uliyotokea kutokana na jaribio la marekebisho ya Katiba, wajumbe walioshiriki mazungumzo hayo waliafikiana kuweka sawa baadhi ya vifungu : " Ibara ya 4 ya rasimu ya mkataba inasema rais wa mpito haruhusiwi kugombea katika chaguzi zijazo baada ya serikali ya mpito, yaani uchaguzi wa Wabunge na urais ambao utakamilisha kipindi cha mpito. Tumeafikiana kwamba Ibara hii haipaswi kufanyiwa marekebisho", amesema Luc Marius Ibriga, kiongozi wa shirika la kiraia (Focal) akiwa pia profesa wa sheria ya katiba, kabla ya kusisitiza: "Tumechukua tahadhari ya kuizuia Ibara hiyo ili rais yeyote atakaye kuja baadae asiwezi kuifanyia marekebisho kwa lengo la kugombea katika uchaguzi mwengine".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.