Pata taarifa kuu
MADAGASCAR-SADC-Siasa-Usalama

Madagascar: Ravalomanana hazuiliwi jela bali alindiwa Usalama

Rais wa zamani wa Madagascar. Marc Ravalomanana amezuiliwa jela baada ya kurejea nchini Jumatatu wiki hii akitokea ukimbizini Afrika kusini.

Kikosi cha wanajeshi mbele ya makaazi ya rais wa zamani wa Madagascar, Marc Ravalomanana, wakija kumkamata baada ya kurejea nchini akitokea ukimbizini, Oktoba 13 mwaka 2014
Kikosi cha wanajeshi mbele ya makaazi ya rais wa zamani wa Madagascar, Marc Ravalomanana, wakija kumkamata baada ya kurejea nchini akitokea ukimbizini, Oktoba 13 mwaka 2014 RIJASOLO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Kabla ya kukamatwa, Ravalomanana amezungumza na vyombo vya habari na baadae wafuasi wake ambao wamekua wamekuja kumlaki nyumbani kwake.

Kwa mujibu wa wafuasi wake, rais huyo wa zamani wa Madagascar haruhusiwi kuondoka nyumbani kwake, lakini katika hotuba yake leo Jumatatu jioni, rais wa Madagascar Hery Rajaomarimampianina amethibitisha kwamba Ravalomanana “hajazuiliwa” jela bali amewekwa sehemu ambako “ analindiwa usalama”.

“ Marc Ravalomanana haja kamatwa aidha kuwekwa mbaroni. Amewekwa sehemu ambako analindiwa usalama dhidi ya vitisho vya aina yoyote”, amesema rais Rajaonarimampianina.

Hata hivo kauli hiyo ya rais huyo ni tofauti na hali iliyojitokeza kwenye makaazi ya Ravalomanana wakati wanajesji walipowatawanya wafuasi wa rais huyo wa zamani kwa kutumia mabomu ya kutoa machozi na baadaye kupenya hadi ndani ya nyumba baada ya kubomoa mlango.

Kitendo hicho cha wanajeshi kimewakera wafusi wa Ravalomanana wakibaini kwamba ni jambo la fedheha kuona mtu aliye kuwa rais anafanyiwa dhulma kama hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.