Pata taarifa kuu
RWANDA-BBC-Mauaji ya halaiki

Rwanda: utata waendelea kuibuka kuhusu filamu ya BBC

Kituo cha matangazo cha BBC kimekanusha tuhuma za Rwanda za kuita filamu iliyorushwa na BBC hivi karibuni kwamba inaegemea.

Rais wa Rwanda , Paul Kagame katika mkutano kuhusu uchumi dunia mjini Davos, Januari 24 mwaka 2014.
Rais wa Rwanda , Paul Kagame katika mkutano kuhusu uchumi dunia mjini Davos, Januari 24 mwaka 2014. REUTERS/Ruben Sprich
Matangazo ya kibiashara

Oktoba 1 mwaka 2014, BBC ilirusha hewani filamu iliyoiita, historia ya Rwanda ambayo haijawahi kuzungumziwa, ambayo inamhusisha rais wa Rwanda Paul Kagame katika mauaji mbalimbali yaliyotekelezwa nchini Rwanda, hususan shambulio dhidi ya ndege aliyokuemo hayati rais Juvénal Habyarimana mwaka 1994, mauaji ya halaiki mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na mauaji mengine dhidi ya wanasiasa waliojitenga naye.

Filamu hiyo imelalamikiwa na shirika la manusura wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda Ibuka, huku ikipongezwa na vyama vingi vya upinzani na msirika ya kiraia yaliyo ukimbizini.

Wakosoaji wa serikali ya Rwanda wana imani kwamba filamu hii inaweza kufungua mazungumzo kuhusu historia ya Rwanda.

"Jumuiya ya raia wa Rwanda waishio Uingereza, kutoka tabaka mbalimbali, vyama vya siasa, maashirika ya manusura, wanaharakati wa haki za binadamu, wameipongeza BBC kwa jitihada zake za kutaka Wanyarwanda kuketi kwenye meza ya mazungumzo na kujadili juu ya kile kilichotokea wakati wa mauaji ya kimbari, na katika mika ishirini iliyofuata" .

Maneno hayo yaliandikwa kwenye mtandao wa shirika la haki za binadamu ( Global Campaign for Rwandan Human Rights), linaloongozwa na mwanaharakati René Mugenzi, mmoja wa raia wa Rwanda wanaoishi ukimbizini tangu mwaka 2011, aliye wahi kupokea ujumbe wa Scotland Yard, na ambaye aliwahi kufanyiwa vitisho vya kuuawa na utawala wa Paul Kagame, kulingana na taarifa alizopewa na polisi ya London.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.