Pata taarifa kuu
PALESTINA-ISRAELI-MISRI-HAMAS-Usalama

Makubaliano ya kusitisha mapigano Gaza: Misri yajizolea sifa na umaarufu

Israel na Hamas wamefikia jumanne wiki hii makubaliano ya kusitiha mapigano, baada ya siku 80 ya mapigano yaliyosababisha vifo vya wapalestina zaidi ya 2000 na zaidi ya 50 nchini Israel. Raia wa Gaza wamedhihirisha furaha yao, huku Umoja wa Mataifa ukipngeza juhudi ilizoanzisha kwa ushirikianao na nchi za Misri na Marekani.

Bendera ya kijani ya Hamas ilipepea jumanne wiki hii nchini Palestina, baada ya tangazo la makubaliano ya kusitisha mapigano.
Bendera ya kijani ya Hamas ilipepea jumanne wiki hii nchini Palestina, baada ya tangazo la makubaliano ya kusitisha mapigano. REUTERS/Ahmed Zakot
Matangazo ya kibiashara

Misri, ambayo imekua ikisimamia mazungumzo ya pande hizo mbili katika mji mkuu wa nchi hiyo, Cairo, imejipongeza kuona imefikia kuwapatanisha waisrael na wapalestina.

Awali mazungumzo hayo yalikabiliwa na changa moto nyingi, hususan mgawanyiko kati ya wapalestina kuhusu ujumbe unaopaswa kuwakilisha kundi la Hamas na lile la Fatah katika mazungumzo hayo, madai ya Israel ya kuwapokonya silaha wapiganaji wa Hamas kabla ya mazungumzo hayo kuanza, pamoja pia na madai ya wapalestina kuomba kuondolewa vizuizi waliyowekewa na Israel katika ukanda wa Gaza.

Hata hivo kulikueko na hali ya sintofahamu baada ya makubaliano hayo kuonekana kutoridhisha baadhi ya wajumbe katika mazungumzo hayo, huku hali ya kubadilika badilika ikionekana kwa pande zote, ikiwa upande wa Palestina aidha Israeli. Wakati huo huo milio ya risase ilikua ikisikika, huku makombora na mabomu vikirushwa na pande zote husika katika mgogoro huo wakati mazungumzo yalikua yakiendelea.

Ujumbe wa Israel katika mazungumzo ya kusitisha mapigano katika ukanda wa gaza, walikua hawawezi kukubali aidha kukataa jambo lolote kabla ya kukutana na Baraza la Usalama la Israel, ambalo kwa sehemu kubwa linaongozwa jeshi.

Upande wa ujumbe wa Hamas ukishindwa kuchukua uamzi kabla ya kukutana kwa mazungumzo na tawi la kijeshi la kundi hilo. Upande mwengine Qatar ambayo inafadhili kundi la Hamas, awali ilipinga Misri kusimamia mazungumzo hayo, lakini ilikuja kukubali wiki iliyopita baada ya mkutano uliyowajumuisha mawaziri wa mambo ya nje kutoka Misri Saudia Arabia, Falme za Kiarabu upande mmoja na Qatar, upande mwengine.

Iwapo makubaliano hayo, hususan mpango uliyoandaliwa na Misri kwa minajili ya mchakato wa amani wa Palestina utatekelezwa, kuna uwezekano wa rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas awe na mamlaka kamili katika ukanda wa Gaza, ambapo alifukuzwa baada ya Hamas kudhibiti eneo hilo mwaka 2007.

Jitihada za Misri za kuanzisha mazungumzo kati ya Palestina na Israel zilianzishwa bila hata hivo Marekani kupewa taarifa. Waziri wa Marekani mwenye dhamana ya mambo ya nje alijaribu kukutanisha pande hizo mbili, bila mafanikio. Katika tangazo liliyotolewa na Marekani, John Kerry amepongeza hatua hiyo ya makubaliano, na kuzitaka pande husika kuheshimu makubaliano hayo, huku akiahidi kuungwa mkono na Marekani.

John Kerry ameelezea matumaini yake kuona makubaliano hayo kati ya Israel na Palestina yanadumu na kupelekea machafuko katika ukanda wa Gaza yanakomeshwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.