Pata taarifa kuu
MALI-MNLA-Mazungumzo

Mali : mazungumzo kati ya serikali na makundi yenye silaha yaanza

Wajumbe wa serikali ya Mali wanatarajia kukutana jumatano wiki hii mjini Algeirs na wawakilishi kutoka makundi ya wapiganaji wa kiarabu katika mazungumzo ya amani kuhusu mustakabali wa nchi ya Mali.

Wajumbe wa waasi wa kituareg  waanza mazungumxzo na serikali ya Mali katika mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou.
Wajumbe wa waasi wa kituareg waanza mazungumxzo na serikali ya Mali katika mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou. AFP/AHMED OUOBA
Matangazo ya kibiashara

Haya yanajiri wakati mashirika yenye kutetea haki za binadamu nchini humo yamethibitisha kuwa serikali ya Bamako iliwaacha huru wafungwa themanini na sita miongoni mwao wanajeshi arobaini na watano wakiwemo polisi walioasi, lakini pia wapiganaji arobaini na mmoja wa kituareg.

Maafisa wa umoja wa mataifa nchini Mali wamesema kuna matumaini ya kufikia mwafaka katika mazungumzo haya, yanayofanyika baada ya kufikia makubaliano ya mwanzo mwezi juni mwaka uliopita mjini Ouagadougou, nchini Burkina Faso.

Mazungumzo hayo yanayotazamiwa kufanyika katika mji mkuu wa Algeria, Algeirs, ni ya kwanza kukutanisha pande zote zinazohusika katika mzozo unaoendelea tangu yale yaliyopelewkea kupatikana kwa mkataba wa muda Juni 18 mwaka 2013 mjini Ouagadougou, nchini Burkina Faso.

Serikali ya Mali imebadilishana mateka na makundi ya waasi wa Mali kabla ya mazungumzo kuanza, Jumanne Julai 15 .
Serikali ya Mali imebadilishana mateka na makundi ya waasi wa Mali kabla ya mazungumzo kuanza, Jumanne Julai 15 . REUTERS/Adama Diarra

Mazungumzo hayo ndiyo yalifungua njia ya kufanyika kwa uchaguzi wa urais na wa wabunge nchini Mali.
Hadi sasa hali ya usalama bado inaendelea kudorora licha ya kuwepo kwa majeshi ya kimataifa.
Tangu kuchaguliwa kwa rais Ibrahim Boubacakar Keïta mwezi Ogasti mwaka 2013, mazungumzo yamekwama, huku makundi yenye silaha yakiendelea na mashambulizi ya hapa na pale kaskazini mwa Mali.

Jumatatu wiki hii mwanajeshi wa Ufaransa aliuawa na wengine saba kujeruhiwa katika shambulio la kujitoa muhanga katika mkoa wa Gao (kaskazini), wizara ya ulinzi ya Ufaransa imethibitisha.

Mwanajeshi huu ametimiza idadi ya ya wanajeshi tisa wa Ufaransa ambao wameuawa tangu ianzishwe operesheni iliyoitwa 'Serval” Januari mwaka 2013.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.