Pata taarifa kuu
MALI

Wapiganaji nchini Mali Waonywa kuchangia upatikanaji wa amani

Umoja wa mataifa Umoja wa Mataifa jana jumatano umetoa wito kwa makundi ya waasi kaskazini mwa Mali na serikali ya Bamako kuanzisha mara moja mazungumzo ya kisiasa na kusisitiza kuwa hali kama ilivyo nchini humo haikubaliki.

Kundi la Wapiganaji wa Kiisilamu la Mujao, eneo la Kaskazini mwa Mali Aprili 12 2013
Kundi la Wapiganaji wa Kiisilamu la Mujao, eneo la Kaskazini mwa Mali Aprili 12 2013 RFI
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Umoja huo, tangu makubaliano ya awali iliyofikiwa baina ya serikali ya Mali na waasi wa Tuareg mwaka mmoja uliopita mafanikio ya mazungumzo hayo yameonekana kuwa finyu tofauti na yalivyotarajiwa.

Hata hivyo, serikali ya Mali kwa upande wake imeomba mamlaka na idadi ya askari wa kulinda amani nchini humo MINUSMA kuongezwa ili kukabiliana na uasi iliokithiri kaskazini mwa Mali kama alivyobainisha waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Abdoulaye Diop,

Mkuu wa operesheni za kulinda amani wa Umoja wa Mataifa UN, Herve Ladsous ameliambia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa hapo jana kuwa mazungumzo pekee baiana ya serikali na makundi hayo ya wapiganaji ndio njia ya kupata suluhu la kisiasa na kuongeza kuwa hali tete ya usalama inayoshuhudiwa sasa nchini humo haikubaliki.

Onyo hili linatolewa siku chache baada ya kushuhudiwa mapigano makali kati ya jeshi la Mali na wapiganaji wa kiisilamu wa toureg katika eneo la Kidal kaskazini mwa nchi hiyo, ambapo jeshi lilishindwa kumudu wapiganaji hao walioudhibiti mji wa Kidal kwa muda wa zaidi ya mwezi sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.