Pata taarifa kuu
SENEGAL

Ofisi ya mwendesha mashtaka ya Ufaransa yasitisha uchunguzi katika kesi ya Abdoulaye Wade, mwana wa raisi wa zamani wa Senegal

Ofisi ya mwendesha mashtaka nchini Ufaransa Jumanne ya wiki hii imetangaza kusitisha uchunguzi dhidi ya tuhuma za rushwa zilizokuwa zinamkabili mtoto wa rais wa zamani wa Senegal, Abdoulaye Wade, mawakili wake wamesema.

Karim Wade akishiriki mkutano wa chama cha PDS, kinachoongozwa na baba yake Abdoulaye Wade, mjini Dakar, desemba 6 2012
Karim Wade akishiriki mkutano wa chama cha PDS, kinachoongozwa na baba yake Abdoulaye Wade, mjini Dakar, desemba 6 2012 REUTERS/Joe Penney/
Matangazo ya kibiashara

Karim Wade ambaye anashtakiwa nchini mwake kwa kujipatia utajiri wa mamilioni ya fedha wakati wa utawala wa baba yake anatarajiwa kupandishwa kizimbani majuma kadhaa yajayo kujibu tuhuma zinazomkabili.

Mwaka 2012 serikali ya Senegal ilipeleka maombi kwa nchi ya Ufaransa kuchunguza tuhuma za rushwa dhidi ya Karim, ikiamini kuwa sehemu ya fedha zinazokadiriwa kufikia euro milioni 170 ziliwekezwa nchini humo na familia ya Wade.

Karim amekuwa kizuizini kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa akituhumiwa kumiliki makampuni na magari yenye thamani ya dola za Marekani, bilioni 1.4.

Uchunguzi kuhusu tuhuma zinazomkabili Karim Wade ziliendeshwa kwa muda wa miaka miwili, huku akiziwiliwa jela kwa kipindi cha mwaka moja sasa.

Awali, waendesha uchunguzi walitafuta ushahidi kuhusu jumba la kifahari lenye thamani ya karibu Uro milioni moja, na baadae iliongezwa tuhuma nyingine inayomuhusisha kumiliki akaunti zaidi ya ishirini mjini Monaco, nchini Ufaransa.

Uchunguzi huo ndio ulisababisha kifungo cha muda kinaongezwa.
Kwa sasa, chanzo kiliyo karibu na faili hii, wanajua kwamba Karim Wade atafikishwa mbele ya mahakama husika inayopamabana na utajiri usiyo halali miezi miwili ijayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.