rfi

Hewani
  • RFI Kiswahili
  • Sikiliza taarifa ya Habari
  • RFI kwa Kifaransa

Uganda Benki ya Dunia WB

Imechapishwa • Imehaririwa

Uganda yaishutumu Benki ya Dunia kwa usaliti

media
Msemaji wa serikali ya Uganda Ofwono Opondo izuba-rirashe.com

Serikali ya Uganda imeituhumu Benki ya dunia kwa usaliti, baada ya Taasisi hiyo ya fedha duniani kusitisha mkopo wa dola milioni 90 kwa nchi ya Uganda kufuatia nchi hiyo kupitisha sheria kali dhidi ya ushoga.


Msemaji wa serikali ya Uganda Ofwono Opondo amesema kupitia kwenye mtandao wa twiter, kwamba benki ya dunia ni taasisi ya mataifa mbalimbali hivyo haipaswi kuwasaliti wanachama wake hata kama ni wadogo kiasi gani.

Siku ya Alhamisi Benki ya Dunia ilitangaza kusitisha mkopo wa dola milioni 90 uliolenga kuisaidia nchi ya Uganda kuimarisha mfumo wake wa afya baada ya Rais Yoweri Museveni kusaini sheria kali ya kupinga vitendo vya ushoga nchini Uganda.

Hata hivyo Uganda imesema haitatishika na vitisho vya mataifa ya Magharibi kuhusu kusitisha misaada yake nchini humo kufuatia kupitishwa kwa sheria hiyo.