Pata taarifa kuu
MADAGASCAR

Uchaguzi wa urais nchini Madagascar wasifiwa kuwa huru na haki

 Waangalizi wa Kimataifa wanasema Uchaguzi wa urais nchini Madagascar umekuwa huru na haki.

Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa waangalizi kutoka Umoja wa Ulaya Maria Muniz de Urquiza, amesema kuwa licha ya kutokea kwa matukio machache ya machafuko zoezi hilo limekwenda vizuri sana.

Kauli hiyo ya waangalizi wa Kimataifa inakuja kipindi hiki Tume ya Uchaguzi ikianza kutangaza matokeo ya awali baada ya kukamilika kwa zoezi hilo siku ya Ijumaa wiki iliyopita.

Matokeo ya awali yanaonesha kuwa mshirika wa karibu wa rais wa zamani aliyepinduliwa mwaka 2009 Marc Ravalomanana,  Richard Jean-Louis Robinson anaongoza kwa asilimia 30 kwa mujibu wa kura zilizohesabiwa hadi sasa huku mpinzani wake wa karibu Hery Martial Rakotoarimanana Rajaonarimampianina akiwa na asilimia 15.

Tume ya Uchaguzi ambayo haijatoa tarehe rasmi ya kutangaza matokeo ya mwisho inasema kuwa matokeo ya mwisho huenda yakafahamika kufikia mwisho mwa mwezi huu.

Ikiwa hakutakuwa na mshindi wa uchaguzi huo atayepata ushindi wa asilimia 50 katika mzunguko wa kwanza, kutakuwa na duru ya pili ya uchaguzi huo tarehe 20 mwezi Desemba.

Wananchi wapatao Milioni 7 walishiriki katika Uchaguzi huo wa urais unaowaniwa na wagombea 33.

Rais wa sasa Andy Rajoelina na yule wa zamani Marc Ravalomanana walizuiliwa na Umoja wa nchi za Kusini mwa Afrika SADC kuwania urais  kwa sababu za kisiasa na usalama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.