Pata taarifa kuu
SUDAN

Takribani watu 29 wapoteza maisha tangu kuanza kwa maandamano nchini Sudani

Takribani watu 29 wameuwawa katika maeneo mbalimbali nchini Sudani katika siku tatu za maandamano kupinga uamuzi wa serikali kupandisha maradufu bei ya mafuta vyanzo vya kitabibu vimearifu. 

Vurugu zikiendelea nchini Sudani
Vurugu zikiendelea nchini Sudani southernminn.com
Matangazo ya kibiashara

Maofisa wa idara ya afya wameeleza kuwa wamepokea miili ya watu 21 tangu kuanza kwa maandamano siku ya Jumatatu, huku mashuhuda wengine wakiarifu kuuwawa kwa watu wengine nane katika miji mingine.

Wanaharakati nchini humo wameitisha maandamano mapya hii leo kwenye mji wa Khartoum kupinga kupanda maradufu kwa bei ya mafuta wakati huu Serikali ikiapa kukabiliana na maandamano hayo.

Maandamano haya yanatajwa kuwa makubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa nchini humo tangu rais Bashir aingie madarakani mwaka 1989.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.