Pata taarifa kuu
ZIMBABWE

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe arejea nyumbani baada ya kupatiwa matibabu Nchini Singapore

Rais Mkongwe wa Zimbabwe Robert Gabriel Mugabe amerejea nchini mwake kutoka Singapore alikokuwa anapatiwa matibabu na kupokelewa kwenye Uwanja wa Ndege wa Harare na kupokelewa na Viongozi kadhaa wakiongozwa na anayetajwa kuwa mrithi wake Makamu wa Rais Joice Majuru.

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ambaye amerejea Harare baada ya kupatiwa matibabu nchini Singapore
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ambaye amerejea Harare baada ya kupatiwa matibabu nchini Singapore
Matangazo ya kibiashara

Rais Mugabe amewasili na kupata mapokezi ya kipekee kutoka kwa Viongozi wa serikali huku afya yake ikionekana imeimarika tofauti na taarifa za awali zilizokuwa zinasema Kiongozi huyo wakati anapatiwa matibabu nchini Singapore hali yake ilikuwa mbaya na kufikia kipindi alikuwa anapambana na umauti.

Bada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Harare Rais Mugabe hakuzungumza na Waandishi wa habari na badala yake aliondoka akiwa kwenye msafara kuelekea kwenye makazi yake kwa ajili ya kupumzika baada ya kupata matibabu nchini Singapore.

Waziri wa Habari wa Zimbabwe Webster Shamu aliwaambia wanahabari Rais Mugabe amerejea nchini Zimbabwe kwa kuwa hali yake ya kiafya imeimarika na hivyo yupo tayari kuendelea na majukumu ambayo yanamkabili.

Waziri Shamu hakuacha kuonesha hasira zake kwa wote ambao wamekuwa mstari wa mbele kumuombea mabaya Rais Mubage na kuhoji ni kwa nini wamekuwa wakipenda kueneza uzushi badalaya kutafuta taarifa zenye uhakika.

Shamu akatumia fursa hiyo kuwashukia wanahabari ambao bado wanaongozwa na mfumo wa Kibepari kuacha kutumia kwenye masuala ambayo ni muhimu kwa taifa na badala yake wafanyekazi kulingana na weledi.

Mapema juma hili Gazeti la Zimbabwe Mail lilitoa taarifa ya kuwa Rais Mugabe yupo katika hali mbaya kiafya akipambana na umauti na ameshakubaliana na Waziri wa Ulinzi Emmerson Mnangagwa achukue madaraka kwa sasa.

Taarifa hizo zilikanushwa vikali na kuitwa uzushi kupitia Waziri wa Habari Shamu ambaye alisema Kiongozi huyo anaendelea vyema huku akisema mara kadhaa Rais Mugabe amekuwa akienda Singapore kupatiwa matibabu.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.